krisi bila hela

Sherehe za krismasi zikianza kushika kasi wakaazi wa kaunti hii ya Uasin gishu wanasema kuwa wanakosa la kusherehekea kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha.

Wakaazi sasa wanasema kuwa hawatasafiri kuelekea mashinani kama ilivyokuwa katika miaka za awali kufuatia kupanda kwa nauli na badala yake wataendelea na maandalizi ya kuwalipia wanao karo ifikiapo Januari mwakani.

Wametoa wito kwa serikali kushughilikia upesi swala la ghrama ya maisha ambayo kwa sasa imewaathiri kibiashara wakisema kuwa hali hii huenda ikapelekea wengi kukosa hada kumudu gharama ya masomo wanafunzi wa kidato cha kwanza wakitarajia kujiungana shule mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *