Tishio la Vitabu ghushi Eldoret

Wazazi katika kaunti ya Uasin Gishu wamelalamikia kulaghaiwa kwa baadhi ya maduka ya kuuzia vitabu na bidhaa nyingine ya mashule.

Wazazi hao walidai kuwa wanauziwa vitabu ghushi na pindi tu wanapofika shuleni wanaarifiwa kuwa vitabu hivyo si halali, kwani ni tofauti na inavyohitajika jambo ambalo limesababisha wanafunzi wengi kurejeshwa ili kununua vitabu vingine.

Walitoa wito kwa wizara ya elimu kuwapa mwelekeo hasa kuhusu vitabu vinavyohitajika ili kuepuka mkanganyiko zaidi.

Hata hivyo wauzaji katika maduka hayo wamekana madai ya ulaghai na kusema kwamba vitabu wanavyouza ni halali wahoji kuwa wamebuni mbinu ambayo wazazi watatumia kutambua vitabu hivyo ni halali au la.

Wauzaji hao walidai kwamba wazazi wameshindwa kutambua aina ya vitabu vinavyohitajika iwapo nit oleo jipya ama la kale, wakisema kuwa hilo ndilo swala pekee linaloleta mkanganyiko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *