NUKUU ISIVYO

Maaskofu wa kanisa katoliki wanazidi kufafanua kile baba mtakatifu Francisko alimaanisha na waraka wake kwa dunia nzima kuhusu baraka ambayo ulinukuliwa visivyo.

Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka amesema kuwa Baba mtakatifu Francisko alieleza kwa kina katika waraka huo kuwa baraka ni kwa wakristu wote na kamwe mtu asibaguliwe kwa msingi ya mapokeo yake kitabia akisisitiza kuwa kamwe kanisa halitaunganisha ndoa ya jinsia moja.

Askofu huyo kadhalika ametoa wito kwa familia kuzungumzia kwa ujasiri maswala hayo ya ndoa na wanao ili wasije wakapotoshwa na wale walio na nia ya kuvuruga kizazi kijacho na kwenda kinyume na mafunzo ya kidini. Amewataka wakenya kutokubali kupotoshwa na kasumba na tabia za kigeni ambayo yananuia kuwafumba wakenya macho kwa kigezo cha kupata ufadhili akiwataka wakenya kutokubali ufadhili sampuli hiyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *