kanda lenye amani

Mbunge mteule wa chama cha UDA Joseph Wainaina amepongeza hatua ambazo wakaazi wa bonde la ufa wamechukua ili kuishi kwa amani na maridhiano.

Akizungumza mjini Eldoret Wainaina ameshabikia matunda ya hamasisho la umma kuhusu amani ambayo anasema kuwa umeibua ufanisi mkubwa miongoni mwa jamii zinazoishi katika eneo pana la bonde la ufa.

Amesema kuwa wananchi wamejifunza mengi kutokana na machafuko yaliyoshuhudiwa nchini baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.

Mbunge huyo kadhalika amewataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi kwenye miji zilizoko kwenye eneo hilo akohoji kuwa kwa sasa bonde la ufa ni tulivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *