Viongozi kwenye kaunti ya Uasin Gishu wametaka uchunguzi zaidi kufanyikia ili kubaini yale yaliyopelekea maafa ya vijana kumi katika zoezi la upashaji tohara.
Akizungumza kwenye sherehe ya Jamhuri katika uwanja wa shile ya msingi ya Chepkigen kaunti ndogo ya Soy kamishna wa kaunti ya Uasin gishu Edison Nyale amewataka machifu kumakinikia zoezi hilo la kitamaduni la upashaji tohara kwa kuwaongoza wananchi katika taratibu zinazofaa.
Naibu gavana wa kaunti ya Uasin gishu Mhandisi John Barorot amesema kuwa jambo zoezi hilo la upashaji tohara linafaa kufanywa kitamaduni amewataka wazee kwa ushirikiano na makanisa na sekta ya afya kushirikiana ili kubaini ni njia ipi zoezi hilo linawezafanya bila majeruhi na maafa jinsi ilivyoshuhudiwa mwaka huu.
Ametoa wito kwa jamii kutoshirikisha watoto wadogo kwenye zeozi hilo akisema kuwa hiyo ndio njia mojawapo ya sababu ambazo huenda ikapelekea maafa.