Mabruda wametakiwa kuwa mashuhuda wema wa uenezwaji wa injili katika taifa la Mungu.
Akihubiri katika Misa ya nadhiri ya kwanza na ya mwisho ya manovisi na mabruda wa shirika la mtakatifu Patrick katika kanisa la mtakatifu Monica RTS askofu wa jimbo katoliki la Kitale Henry Juma amewataka mabruda hao kuwa chumvi za Dunia kwa kuipa tumaini taifa la Mungu na kuwa waaminifu kwa wito wao.
Askofu Juma amesema kuwa wito wa ubruda unachangamoto si haba akitoa wito kwao kumtanguliza kristu siku zote ili awaongoze akitoa wito kwa wakristu kadhalika kuwaombea ili wito huo uweze kuenea.
Mabruda ambao wamepokea nadhiri za mwisho ni Thomas masese, Benard Oseko, Gilbert Kipkorir huku manovisi ambao wamepokea nadhiri za kwanza wakiwa Gabriel Magero, Sylvester Chimwanga na Brian Nyerere