Kanisa linapoanza kipindi cha maajilio wakenya wametakiwa kudumisha amani ma kujirudia kama njia moja ya kunyoosha mapito yake mkombozi.
Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret amesema kuwa hiki ni kipindi cha kila mmoja kutafakari maisha yake na kujirudia kama njia moja ya kujiandaa kupokea kristu ili azaliwe mioyoni mwao akitoa wito kwa kila mmoja kuhubiri amani msumu huu.
Askofu kadhalika amewataka vijana kuwa makini haswa katika msimu huu wa sherehe ili wasije wakanaswa na mambo ambayo yatawaharibia maisha ya siku za baadaye kama matumizi ya dawa za kulevya, na kujiingiza katika maswala ya ngono na badala yake wajifunge nira ya kujihusisha na warsha mmbalimbali za kanisa ambayo zitawajenga kiimani.
Amewapa wazazi cahangamoto ya kuwaonyesha wanao upendo akisema kuwa upendo kutoka kwa mzazi hujenga maadili kwa watoto hao na kdhalika kuwapa msingi dhabiti wa kuwa na uwezo wa kujiamulia yale mazuri.
