Askofu mkuu wa kanisa la Kiangilikana Jackson Ole Sapit ameeleza haja ya juhudi zaidi kuwekwa za kuhakikisha mtoto mvulana anapata elimu, hii anasema ni kutokana na kuendelea kutelekezwa kwa watoto wa kiume.
Askofu Ole Sapit amewataka wadau wote nchini kuungana na kuhakikisha kwamba motto mvulana haachwi nyumba kwa kuwa juhudi za kumuinua mtoto msichana zimefaulu huku mvulana akiachwa nyuma akitoa wito kwa serikali kadhalika kuingilia kati swala hili ili mtoto wa kike na wakiume waangaziwe kwa usawa.
Ametoa wito kwa jamii za wafugaji kukoma kushikilia mila ambayo anasema zimeendelea kurudisha nyuma juhudi za kumuinua mtoto mvulana akihoji kuwa vijana wengi wameacha masomo ili kufuatilia mila hizo.
Amedokeza kuwa swala la utandawazi kadhalika limeteka jamii akitoa wito kwa kila jamii kuhakikisha kuwa inaendana na mawimbi haya ya utandawazi.