mshukiwa wa mauaji ahukumiwa miaka 45

Familia ya aliyekuwa mwanafunzi wa chuo Cha urembo Mjini Eldoret Vera Emma Wanyota imesema imeridhika na uamuzi wa Mahakama kuu ya kumhukumu Mustapha Idd miaka 45 Jela kwa kumuua mwana wao.


Wakiongozwa na mama yake mwendazake na pacha wa marehemu Sharon Wanyota wamesema kwamba angalau mwana wao atapata haki na unyama  huo utaweza kutokomezwa.

Yanajiri haya baada ya mahakama kuu ya Eldoret ilimhukumu Mustafaha Idd mwenye umri wa miaka 40 jela miaka 45 kwa kupatikana na hatia ya kumuua Emma Wanyota aliyekuwa mwanafunzi wa chuo Cha urembo Cha Vera.


Akitoa hukumu hiyo Jaji Reuben Nyakundi ametaja kitendo hicho kama Cha unyama na mshukiwa huyo alistahili kuhukumiwa kifungo Cha kunyongwa iwapo katiba ingeruhusu hatua hiyo.

Upande wa mashtaka wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo mshukiwa huyo alimuua kikatili Emma Wanyota mwanafunzi wa chuo Cha urembo Cha Vera mnamo Septemba 30 2019 baada ya mwili wa mwendazake kupatikana kichakani katika eneo la Moi’s Bridge huku mwili wake ukiwa umetanganishwa na miguu, mikono na baadhi ya viingo vyake.


Hadi kuhukumiwa kwake,Mustapha alikana shtaka dhidi yake.


Ana siku 14 kukata rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *