Wakaazi wanaoishi katika maeneo ambayo yako kwenye hatari ya kukumbwa na maporomoko ya ardhi wanafaa kuhamishwa mara moja ili kuepuka athari zaidi za mvua ya Elnino.
Akitoa agizo hilo wakati wa kikao cha dharura kwenye ikulu jijini Nairobi rais William Ruto alisema kuwa tayari watabiri wa idara ya hali ya anga wametoa tahadhari nchini kuwa mvua itaendelea kunyesha katika kipindi cha siku saba zijazo, na kuendelea hadi mwisho mwisho wa mwezi wa January mwaka ujao.
Rais Ruto kadhalika alitoa wito kwa wakulima katika maeneo ambayo yanapokea mvua ya kadri kutumia mvua hiyo kukuza mimea tofauti tofauti ili kusaidia taifa kukabili uhaba wa chakula nchini.