Wanakwaya kote jimboni wametakiwa kuiga mfano wa somo wao ambaye ni mtakatifu Cecilia kwa kuwa mfano Bora na Baraka katika maisha ya wakristu.
Akihubiri katika kanisa la moyo mtakatifu wa Yesu kathedrali kwenye Misa ya kusherehekea siku ya mtakatifu Cecilia chansela wa sekretarieti ya jimbo padre Vincent Kitur alitoa wito kwa Kila mwanakwaya kujisadaka bila kujibakisha katika uimbaji huo akisema kuwa kwaya ni kiungo muhimu katika liturjia.
Alitoa wito kwao kujinyima ili kuurithi ufalme wa mbingu katika maisha yajayo akisema kuwa kule kujinyima huwezesha muimbaji kuwa mfano Bora na chombo cha Baraka katika nyoyo za Waumini.
Padre Kitur kadhalika aliwataka waimbaji hao kukumbatia msamaha kama ngao ya kujikinga dhidi ya maovu ambayo yanaleta misukosuko ndani ya kikundi hicho cha kwaya.