Hamasisho ya Ufisadi Eldoret

Tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC imeandaa warsha na magavana kama njia moja ya kuwahamasisha serikali za gatuzi kuhusu ufisadi ambao kwa sasa umekithiri katika kaunti mbalimbali nchini.

Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim amepongeza hatua ya ushirikiano kati ya serikali za gatuzi na tume hiyo ya kupambana na ufisadi akisema hiyo ni mbinu mwafaka wa kupiga jeki vita dhidi ya jinamizi la ufisadi ambayo kwa sasa kulingana na ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali inasema kuwa imekithiri katika kaunti mbalimbali.

Naye gavana wa kaunti ya Kisumu profesa Anyang Nyongo ametoa wito kwa tume hiyo kukaza kamba dhidi ya unyakuzi wa ardhi ya umma katika kaunti mbalimbli nchini akisema kuwa swala hili limezua vuta nikuvute kati serikali hizo za gatuzi na watu binafsi walionyakua ardhi hizo.

Maneja wa tume hiyo ukanda wa kaskazini mwa bonde la ufa Charles Rasugu amesema kuwa hatua hii inalenga kuboresha uhusiano bora wa kikazi katik ya tume yake na serikali hizo akisema kuwa ushirikiano huo tayari imepelekea tume hiyo kurejesha ardhi zilizonyakuliwa za kima cha shilingi bilioni saba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *