Umoja wa jimbo la Kakamega

Askofu wa jimbo katoliki la Bungoma Mark Kadima ametoa wito amani miongoni mwa wakristu kama njia moja ya kufanikisha mshikamano wa taifa.

Akihubiri katika sherehe ya family day jimbo katoliki la Kakamega askofu Kadima aliwataka wakristu kujiepusha na maswala ambayo huenda yakazua mgawanyiko miongoni mwa jamii akisema kuwa uchochezi, fitina na masengenyo ndio maswala kuu ambayo huyumbisha umoja na mshikamano miongoni mwa jamii.

Askofu huyo kadhalika aliwataka wakristu siko zote kuwa wakarimu akisema kuwa tabia ya kuwa mkono ghamu huenda ikamnyima mkristu baraka ya kumiliki mali, akitoa wito kwa kila mmoja kushirikiana na wenzao katika utekelezwaji wa miradi mbalimbali.

Alitoa wito kwa kila mmoja katekeleza wajibu wake kwa usawa bila ubaguzi akisema kuwa ubaguzi kwa msingi ya kikabila ni miongoni mwa mambo yanayorudisha taifa nyuma kimaendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *