Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameitaka serikali ya kitaifa kupitia wizara ya ulinzi wa kitaifa kuwahakikishia usalama wanafunzi hasa walio kwenye maeneo yanaokumbwa na mzozo na vita vya mipaka.
Akizungumza katika shule ya upili ya Bishop Delany wakati wa hafla ya maombi kwa kidato cha nne ,askofu Kimengich aliseieitiza umuhimu wa maafisa wa usalama kuwawekea ulinzi wa kutosha wanafunzi wao ili kusishuhudiwe maafa yoyote au hata kuwaingiza uwoga wanafunzi wanapoendelea na mitihani yao.
Aidha,askohu Kimengich aliwasihi wanafunzi kuwa na matumaini kwenye mtihani huo akiwaeleza kwamba iwapo walijitayarisha vyema watafulu huku akiwataka kukubali matokeo hayo pindi yatakapotolewa.