Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameitaka serikali ya kitaifa kuangazia upya bei ya mahindi ambayo imekwisha tangaza.
Akizungumza mjini Eldoret Askofu Kimengich alisema kwamba yastahili serikali kumjali mkulima ambaye alitumia muda wake pamoja na rasilimali yake kuhakikisha amepata mavuno mazuri.
Alisema kwamba gahrama ya uzalishaji mwaka huu ilikua ya juu mno a sharti serikali kuweka kipaumbele swala hilo la sivyo wakulima wengi watapata hasara na hata kushindwa kurejea mashambani kwa upanzi wa mahindi mwaka ujao kwa kukosa hela.
Kimengich alipendekeza serikali angalau ichukue mavuno ya wakulima wa mahindi kwa shilling elfu sita kwa kilo tisini ya mahindi .
Wakati huo,amesisitiza kwamba kwa sasa gharama ya maisha imepanda na mkenya wa kawaida hususan mkulima amefinyika hata zaidi na hivyo haja ya matakwa yao yazingatiwe maana ukulima ndio uti wa mgongo wa taifa la Kenya.
