Arobaini za watano

Maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kapsoya kaunti ya Uasin Gishu waliwakamata washukiwa watano wa wizi wa magari na vifaa vingine mjini Eldoret na katika viunga vyake.

 Akithibithisha haya kamanda wa Polisi Kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi alisema kwamba washukiwa hao na wengine ambao wanaendelea kusakwa wamekuwa na mazoea ya kupora magari yaliyoegeshwa na kutoweka na vifaa vingine vya waathiriwa.

Vilevile kamanda huyo alieleza kwamba huenda wezi hao wanatekeleza uhalifu huo kaunti hii na kujificha kwenye kaunti jirani.

Aliwapongeza wenyeji kwa kujitolea kwao kuwajuza maafisa wa usalama kuhusu wahalifu akisema hili litasaidia pakubwa kukabili uhalifu.

Mwanthi aliwataka wakaazi kadhalika kujiepusha na biashara ya pombe haramu akieleza kwamba idara ya usalama itaendelea na vita dhidi ya pombe haramu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *