Wakaazi wa eneo la Chemolingot eneo bunge la Tiaty katika kaunti ya Baringo wameombwa kuwa na subri wakati serikali ya kaunti hiyo inashughulikia uhaba wa maji.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa bodi ya maji eneo hilo Kennedy Okeno alisema kwamba uhaba huo wa maji umechangiwa pakubwa na hitilafu za mitambo za kusambaza maji na juhudi zinafanywa kuboresha usambazaji wa maji.
Alisema serikali ya kaunti hiyo ikishirikiana na washikadau kutoka sekta mbalimbali kuhakikisha maji safi inapatikana na wenyeji kuweza kuerejelea kwenye shughuli zao za kawaida.
Aidha,alipinga kinachosemwa kwamba uhaba huo wa maji umechangiwa na kampuni ya kusambaza maji kaunti hiyo iko na deni kubwa chanzo cha kukosekana kwa maji kaunti hiyo akieleza kwamba huo ni uvumi tu.