Walimu wa shule za chekechea kaunti ya Uasin Gishu wamemtaka gavana wa kaunti hii Jonathan Bii Chelilim kuwajumuiisha kwenye mpango wa maziwa ya bila malipo kwa wanafunzi wa chekechea.
Walisema kwamba mpango huo umechangia pakubwa idadi ya wanafunzi kuongezeka hadi kufikia zaidi ya elfu tatu kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwa kuwa mpango wenyewe unatekelezwa katika vituo vyote vya elimu ya masomo ya chekechea na ulizinduliwa rasmi mwezi Mei mwaka huu.
Wanasema kwamba himizo hilo lao la kuhusishwa kwenye mpango huo unatokana na shinikizo la wanafunzi wao kuwataka walimu wanywe maziwa pamoja nao.
Kulingana na afisa mkuu katika idara ya elimu kaunti hii Mario Birgen ni kwamba ombi la walimu hao litaangaziwa iwapo bunge la kaunti litatenga pesa zaidi ya kuongeza kiwango cha maziwa yanayosambazwa kwa shule ili kujumuisha walimu.