ASKOFU RUTO:kuzeni talanta za watoto

Himizo limetolewa kwa wazazi kutambua talanta walizo nazo wana wao na kuwasaidia kuzikuza ili talanta hizo ziweze kuimarishwa.

Akizungumza wakati wa maombi kwa wanafunzi wa darasa la nane na gredi ya sita wa shule ya msingi ya Biribiryet kaunti ya Nandi,askofu wa kianglikana jimbo la Kapsabet Christopher Ruto amesema kwamba ni swala la kuridhisha kuona kwamba kizazi kijacho kina mwelekeo dhabiti wa uongozi kupitia ukuzaji bora wa talanta zao.

Alisema kwamba wazazi wanapaswa kuwasaidia wanao kuweka msingi bora talanta hizo bila ya wao kuwanyoshea kidole ya lawama akiwashauri kwamba kila mtoto alibarikiwa kwa njia tofauti na inawapasa kujua ni yupi ana uwezo kuliko mwingine na hivyo wanapaswa wote kupata nafasi sawa ya kueleweka.

Askofu Ruto kadhalika,aliwakanya wazazi dhidi ya kuwabagua watoto hasa wale ambao wamekosa kupata alama wanazozihitaji kwenye mitihani yao shuleni akiwaeleza wkamba kila mtoto ana uwezo kwa njia tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *