mjitenge na dhana potovu

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret aliwatahadharisha wakistu dhidi ya dhana potovu juu ya sakramenti ya mpaka wa wagonjwa.

Askofu Kimengich alisema kuwa mpako wa wagonjwa ni sakramenti ambayo hupyaisha maisha ya binadamu na hata kutakasa roho ya Yule ambaye amedhoofika kutokana na maradhi mbalimbali, akufutilia dhana kuwa kule kupakwa mafuta hayo niĀ  kuchungulia kaburini, akisema kuwa hii ni njia mojawapo tu ya kutengeneza agano na mwenyezi Mungu kwa lengo la kupata uponyaji.

Kadhalika aliwaonya wakristu dhidi ya kutumia mpako wa wagonjwa kama kinga dhida ya majanga mbalimbali yakiwemo mtu anaposafiri akisema kuwa sala ndio nguzo kuu na kinga dhabiti kwa Yule anayesafiri akiwaonya wakristu dhidi ya kutumia sakramenti hiyo ya mpako wa wagonjwa kama kinga dhidi ya mauti.

Maelezo haya yanakuja wakati ambapo kumekuwa na hisia tofauti na dhana tofauti kuhusu sakramenti hiyo ya mpako wa wagonjwa wengi wakihusisha mpaka wa wagonjwa kama harakati za kujiandaa kufa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *