biashara yashika kasi

Shughuli za biashara katika mji wa Eldoret zimepamba moto huku kongamano la nane la ugatuzi ukiendelea kaunti ya Uasin Gishu kwa siku ya pili.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa muungano wa wafanyibiashara tawi la Uasin Gishu Willy Kenei ni kwamba wafanyibiashara wengi wamenufaika na kuweza kuuza bidhaa zao kwa wateja ambao wamejitokeza mjini Eldoret kwa uwingi.

Kenei amewataka wafanyibiashara kuendelea kujituma wakati kongamano hili linapoendelea ndipo wao pia waweze kujijenga kimaisha.

Mwenyekiti huyo vilevile amesema kwamba vyumba vyote vya kulala vimejaa huku baadhi ya wageni wakilazimika kutafuta malazi nje ya mji.

Kadhalika,amesema kuwa kuna maonyesho ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa kaunti mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *