Jitengeni na ubinafsi

Wito umetolewa kwa wakenya na wakristu kwa jumla kuwa macho kila muda wasije wakajiingiza kwenye maswala ambayo huenda yakawaelekeza kwenye mauti.

Akiongea katika kanisa la Mtakatifu Mathia Mulumba huko Mikindani,askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa ambaye pia ni mwenyekiti wa kongamano la maaskofu wa katoliki nchini KCCB Martin Kivuva Musonde alisema kwamba kuna watu ambao katika maisha yao kila jambo wanayotilia maanani ni kupata kunufaika kupitia njia zisizo stahili swala analosema lapaswa kuepukwa.

Vilevile,askofu Kivuva aliwataka wakristu kujitenga na ubinafsi akieleza kuwa itawafungia nje katika kuutwa ufalme wa mbingu akiwarai kuwa mabalozi wema katika maisha ya ukristu na kuwa mfano mwema kwa wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *