Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich aliwateua mapadre watakaodumu katika sekretarieti ya jimbo, hii ikiwa ni baadhi ya yale yaliyomo kwenye sinodi.
Safari ya sinodi kwa maana kutembea pamoja ilianza na ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wakristu kwenye ngazi ya jumuiya na kisha kilele chake kikawa ni kongomano la sinodi lililoandaliwa mwaka jana kwa lengo la kuanisha yale yaliyokusanywa kutoka kwa wakristu.
Maamuzi hayo yalimpa askofu Mamlaka ya kuwateua wale watakosimamia vitengo mbalimbali katika sekretarieti ya jimbo katika ngazi ya jimbo na hata katika kaunti mbalimbali chini ya jimbo.
Akitoa tangazao hilo askofu Dominic Kimengich amemteua padre inceny Kitur kuwa Chansela wa Jimbo akiwa na jukumu la kuomgoza sekretarieti ya jimbo, idara ya wito sasa itaongozwa na padre Gregory Kimeli huku idara ya mawasiliano sasa ikisimamiwa na padre francis Kamau ambaye anachukua nafasi yake padre Fredirick Njoroge.
Padre Japheth Machichim ameteuliwa kuwa padre mkuu wa eneo pana la Nandi, padre Stephen Njure akiteuliwa kuwa padre mkuu wa Uasin gishu Elgeiyo marakwet wakipata padre David Mutai Ruto kama padre mkuu wao.
Padre Edwin Kangogo sasa atasimamia idara ya elimu katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet, Kuanti ya Nandi ikisimamiwa na Joseph Limo huku ile ya Uasin Gishu ikisimamiwa na padre Raphael Opondo
Idara ya liturjia jimboni sasa itasimamiwa na padre Sospeter Kangogo.
