Gavana wa kaunti ya Nandi Stephen Sang ameweka bayana kwamba wameweka mikakati kama ukanda wa North Rift kuhakikisha kwamba swala la amani kwenye maeneo tata inaangaziwa.
Akiongea katika hafla ya Family Day katika kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Kathedrali gavana huyo amesema utata ambao umeshuhudiwa wa utovu wa usalama ambayo kwa muda mrefu imewanyima usingizi wenyeji ukanda wa kaskazini mwa Bonde la Ufa unapaswa kuitimishwa na wenyeji maeneo hayo waweze kufurahia matunda ya uwepo wa amani na kuendelea na shughuli zao za kujenga maisha na taifa.
Sang vilevile,ameomba ushirikiano baina ya wenyeji,viongozi wa dini na wa kisiasa ukanda huo kusaidia katika upatikanaji wa amani eneo hilo kwa ukamilifu.
