Bishop Muhatia; Umoja kwa ufanisi wa Jimbo

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muhatia Makumba amewataka wakristu kushirikiana kufanikisha ujenzi wa nyumba ya bwana.

Akiongea wakati wa hafla ya Family Day kwenye uwanja wa Upadrisho wa Moyo Mtakatifu wa Yesu Kathedrali Eldoret,askofu mkuu amewarai wakristu kujitolea kikamilifu kutimiza uinjilishaji kwa watu ambao bado hawajamfahamu mwenyezi mungu kote duniani.

Askofu mkuu vilevile amesisitiza kwamba wakristu wasipochukua jukumu lao kuu la kusaidia watumishi wanaohudumu katika shamba la bwana ,huenda wakazamisha azma ya kuenezwa kwa neno lake kristu kwa mataifa yote hii ikiwa ni kupitia ushirikiano wao wa kujitolea kwa ujnzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kanisani.

Amesema kwamba wakristu wasipo ungana mikono kuendeleza michango kanisani shughuli za ujenzi wa kanisa utaporomoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *