Vijana wameshauriwa kuwa waangalifu na yale wanayofanya au kutuma kwenye mitandao ya kijamii isije ikawa chanzo cha kuwaharibia wengine maisha yao au hata kusababisha utovu wa usalama
Kulingana na mwakilishi wadi wa Kapsaos katika kaunti ya Uasin Gishu Isaac Kibet Samoei ni kwamba mitandao ya kijamii mara si moja imetumiwa vibaya na wakenya akisema kwamba mtandao huo inaweza ikasababisha watu kulumbana au hata kujiingiza kwenye maswala yasiyofaa katika maisha.
Alisisitiza haja ya vijana kujituma kupitia mitando hizo za kijamii kama vile kupata maarifa zaidi au hata kueneza jumbe za amani na matumaini kwa wengine.
Mwakilishi huyo vilevile aliwasahuri vijana kujitenga na marafiki ambao wanaweza wakawaelekeza pabaya kutokana na hulka na mienendo zao akisema kwamba kuna maswala tata ambazo zimejitokeza na kuwalenga vijana swala analosema sharti vijana hao wakue makini mno.
Aidha,aliwataka wazazi kuwa karibu na wanao msimu huu wanapokuwa kwenye likizo ili kuwaelekeza vyema katika maisha.
Wakati huo, alisema katika wadi yake,wamepanga namna ya kuwasaidia vijana kujiepusha na maswala yanayoweza kuwapotosha kwa kuandaa mashindano aina mbalimbali hasa msimu huu wanafunzi wanapokuwa kwenye likizo ndipo waweze kuwa na nidhamu kabla na hata baada ya kurejea shuleni.