Viongozi wa kidini katika kaunti ya Uasin Gishu sasa wanasema kukosa masomo bora ya theolojia kwa baadhi ya wahubiri na viongozi wa dini imechangia pakubwa uwepo wa hulka ya kishetani mingoni mwa madhehebu nchini.
Wakiongozwa na George Gichana wa kanisa la Deliverance na Sheikh Abubakar Bini viongozi hao walisikitia hali ambayo viongozi wa uwongo wamejitokeza na kuwavuruga waumini akili zao kwa dhana potovu ya kutajirika au hata kwenda mbingu mara moja kwa kujinyima chakula swala wanalosema sharti likomeshwa mara moja na maisha ya wakenya ilindwe.
Kadhalika,viongozi hao waliitaka serikali kudhibiti madhehebu yanayojitokeza kwa kubuni sheria kali ili kuwalinda wakenya dhidi ya kuingizwa kwenye njia ya mauti.
Kauli hizi zimetolewa na viongozi hao wa dini kufuatia utata unamzingira Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International Church anayetuhumiwa kuhusika kwa mafundisho potovu ya kufunga hadi kufa kwa waumini wake ndipo wakutane na mungu.