Mapema hii leo rais Uhuru Kenyatta amejiunga katika misa ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya msimu wa kipindi cha Kwaresma ya kanisa katoliki katika madhabau ya Subukia kwenye kaunti ya Nakuru.
Rais pia anatarajiwa kushuhudiwa kuzinduliwa kwa waraka wa maaskofu wa kanisa katoliki ambapo maaskofu hao huwahimiza wakristo pamoja na wahisani kuweza kuungana na kukabiliana na matatizo yanoyokumba jamii wakti wakitetea mabadiliko humu nchini.
Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kufunga, kujinyima, kusali na kutubu kabla ya kipindi cha pasaka kuongoa nanga rasmi. Kipindi hichi huanza jumatano ya majivu na kumalizika jumapili ya matawi ikiwa ni maadhimisho ya kila mwaka huwatayarisha waumini katika kipindi cha toba, kutoa zaka na kujinyima kwa matukio yanayohusiana na mateso ya yesu msalabani na pia maadhimisho ya kufufuka kwake