Wakulima kwenye kaunti ya Uasin gishu hivi karibuni watasafirisha mazao yao sokoni kwa wakati baada ya serikali ya kaunti kuzindua mpango wa kukarabati barabara katika wadi zote kwenye kaunti hiyo.
Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim akiongea kwenye hafla ya kuzindua barabara ya Merewet iliyoko kwenye wadi ya Soy, amekariri kuwa serikali yake ina mpango wa kuhakikisha kuwa barabara kwenye wadi zote zimewekwa lami na halkadhalika kusafisha mitaro yote iliyozibwa na taka kama njia moja ya kuzia mafuriko kwenye barabara wakati wa mvua.
Baadhi ya barabara zitakazokarabatiwa kwa ushirikiano na mamlaka ya kukarabati barabara za miji nchini KURA ni pamoja na barabara ya Bandaptai na ile ya Famers, serikali ikihaidi kuweka mahali pa kutembelea kwa wale watakaotumia miguu ni ile Saroiyot miongoni mwa barabara zingine mjini Eldoret.
Mkurugenzi mkuu wa KURA Silas Kinoti amesema kuwa hatua kukarabati barabara hizo kadhalika zitasaidia kupunguza msongamano wa magari , nah ii itasaidia na kufanikisha bidhaa nyingi kufikishwa sikoni kwa wakati.