Papa Francisko:Kiwango cha upole kinapimwa kupitia magumu!

Heri wenye upole, maana watairithi nchi, ndiyo heri ya tatu ambayo Papa Francisko amejikita nayo katika katekesi yake na kufafanua kwamba hakuna ardhi nzuri zaidi kuliko mioyo ya wengine, hakuna eneo zuri zaidi la kupatikana kwa amani na nduguyo.

Upole unakuwezesha kupata mambo mengi. Upole una uwezo wa kushinda moyo, kuokoa urafiki na mambo mengi, kwa maana watu wanakuwa na hasira lakini baadaye wanatulia, wanafikiria kwa upya na kurudia katika hatua zao za safari na kwa maana hiyo inawezekana kujenga upya urafiki kwa njia ya upole.

Nchi itakayoshinda kwa upole ni wokovu wa huyo ndugu aliyetajwa katika Injili ya Mathayo mwenyewe kwamba: ikiwa atakusikiliza, umempata nduguyo. Papa amesisitiza kwamba hakuna nchi nzuri zaidi ya moyo wa mwingine, lakini tufikire hili kwamba  hakuna ardhi nzuri zaidi kuliko mioyo ya wengine na hakuna eneo zuri zaidi la kupatikana kwa amani na nduguyo. Na ndiyo hiyo nchi itakayorithiwa kwa upole.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *