kaunti yapokea mashine za kufungua barabara

Serikali ya kaunti ya Elgeyo Marakwet  imepokea mashine kutoka shirika  la huduma ya kitaifa  kwa vijana  ambalo litasaidia  kufungua barabara katika maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo.

Akiongea baada ya kupokea mashine hizo  gavana wa kaunti hiyo Wesley Rotich amesema kuwa bado wanatarajia mashine  zingine zitakazotumika kukarabati barabara katika maeneo bunge zote manne za kaunti hiyo .

Rotich aidha alidokeza kuwa  hatua hiyo itawasaidia wakazi hasa kusafirisha  bidhaa zao sokoni  na  kuboresha shuguli za uchukuzi hasa kwa maafisa wa usalama wanaoendeleza oparesheni katika maeneo ya bonde la Kerio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *