Mwanamume mmoja amefikishwa katika mahakama ya Iten Kwa kosa la kumteka nyara mtoto msichana mwenye umri wa miaka 14.
Mbele ya hakimu mwandamizi Charles Kutwa Hillary Kimwetich Biwott alikabiliwa na shtaka kuwa kati ya tarehe 10/10/2021 na 17/10/2021 katika Kijiji Cha Sokoyo katika lokesheni ya Kaptalamwa kaunti ya Elgeyo Marakwet alikuwa na nia ya kusababisha msichana huyo kufichwa kisiri na Kwa kimakosa.
Hillary alikabiliwa na kosa la pili kuwa mnamo tarehe 10/10/2021 katika Kijiji Cha Kapsarbet lokesheni ya Yemit kaunti ya Elgeyo Marakwet alimnajisi msichana huyo kinyume Cha sheria.
Hillary alipopewa nafasi ya kujitetea alikubali mashtaka hayo huku Kiongozi wa mashtaka Judith Ayuma akiomba korti kumpa tarehe ya kujua ukweIi.
Hata hivyo mwanamume huyo anazuiliwa katika gereza la Tambach,kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa mnamo tarehe 26/10/2021.