Jimbo katoliki la Eldoret siku ya Jumamosi liliandaa misa ya shukrani kwa ajili ya askofu mkuu mwandamizi mteule Dominic Kimengich kusherehekea miaka sita ya utumishi katika jimbo hilo.
Askofu wa jimbo katoliki la Kapsabet John Lelei akihubiri katika adhimisho hilo, alimmiminia sifa askofu mkuu Kimengich akitaja baadhi ya mageuzi aliyofanya tangu kuja jimboni mwaka wa 2020.
Askofu altaja miradi mbalimbali kama vile eneo la sala la Kabiyet ujenzi wa st John amani Center na sinodi kama baadhi ya mageuzi aliyofanya jimboni katika miaka hizo.
Askofu Kimengich sasa anatarajiwa kupokelewa kwenye jimbo kuu katoliki la Mombasa jumamosi ijayo sherehe ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na maaskofu wa baraza la maaskofu nchini KCCB.
