Sudi asuta Kahiga na wapambe wake

Matamshi ya gavana wa kaunti ya Nyeri Mutahi kahiga bado yanazidi kukosolewa na viongozi mbalimbali nchini, wakimsuta kwa kushabikia kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi alimsuta gavana huyo kutokana na matamshi yake hivi majuzi, ambayo kulingana na Sudi ni kuwa yanalenga kuleta mgawanyiko wa kikabila nchini.

Akizungumza katika hafla ya mchango kwenye kaunti ya Vihiga Sudi amemtaja Kahiga kama kiongozi ambaye amekosa nidhamu na mwenye roho chafu.

Sudi kadhalika alimkashifu kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, akidai kuwa ndiye mkuu wa viongozi wanaoeneza siasa za ukabila humu nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *