Wito umetolewa kwa wakristu kuwasaidia wengine katika jamii pasi na kuegemea tofauti za kitabaka,kabila au misingi yoyote.
Akihubiri wakati wa sherehe za Family Day Jimbo katoliki la Eldoret kwenye uwanja wa upadrisho ya Kathedrali ya Moyo Mtakatifu wa Yesu,askofu wa jimbo katoliki la Kitale Henry Juma Odonya amesema kwamba watu wengi katika jamii wametengwa na inapasa kwa mkristu kuwa kielelezo chema na kumsaidia, ili wao pia waweze kumjua kristu.
Aidha,askofu Odonya alisisitiza haja ya mkirstu kujisadaka bila ya kujibakisha ili aweze kuutwa ufalme wa mbingu.