Miito ni nguzo muhimu kwa jamii

Wito umetolewa kwa makleri na majandokasisi kuimarisha sala ili  waweze kusimama imara katika uenezwaji wa Injili.

Kwa mujibu wa Askofu wa jimbo jimbo katoliki la Kakamega Joseph Obanyi Sagwe ni kwamba ili watumishi katika shamba la bwana waweze kuistawisha shamba hilo sharti wazo la sala litangulizwe kila wakati.

Kauli ambayo imeungwa mkono na askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ambaye aliwashauri wakristu kuziombea miito mbalimbali ili kanisa iweze kuwapokea watumishi wengi wenye msimamo dhabiti katika kristu.

Kadhalika,padre Michael Rop anayesimia miito kwa mapadre decania ya Nandi alisema wameweka mikakati ya kuhakikisha miito inalindwa katika maeneo ya mashinani na kusaidia katika kuweka hai taifa la bwana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *