Uamuzi uwezi kuwafaa wote

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki  nchini KCCB limeshtumu serikali  likidai kuwa hatua ya serikali kukiuka amri za mahakama huenda  ikaweka taifa hili katika hali utawala wa kiimla.

Katika taarifa iliyotolewa na baraza hilo na kutiwa sahihi na mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Mombasa askofu Martin Kivuva imesema kuwa hali ilivyo kwa sasa ya tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inawanyima wakenya wengi haki ya kuwakilishwa kwa kuwa kuna chaguzi ndogo nyingi ambayo yanastahili kusimamiwa na tume hiyo.

Askofu mkuu kivuva ametoa wito kwa serikali  na jopo husika kuchukulia jambo hilo kama la dharura na kuwateua makamishna akisema kuwa kutokuwepo kwa makamishna hao huenda kikatumbukiza taifa hili katika hali ya sintofahamu.

Hatua hii inajiri punde tu baada ya mahakama kuagiza jopo lililobuniwa na rais WilliamRuto kuendelea na zoezi la uteuzi agizo ambao tayari limepingwa na kiongozi wa upinzani raila Odinga huku viongozi wengine wakipendekeza kuwa kuwe na mikakati maalum kabla ya kuanzishwa kwa mchakato huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *