Gharama ya mlo

Huenda wakulima wengi wa zao la mahindi katika eneo la Kaskazini mwa bonde la ufa wakagharamika zaidi kununua pembejeo licha ya rais William Ruto kuhaidi kupunguza bei ya bidhaa hiyo ili kuwafaidi wakulima.

Kulingana ma mwenyekiti wa wakulima hao katika eneo hili la Kaskazini mwa bonde la Ufa Kipkorir Menjo alisema kuwa huenda wakulima wengi waliosajiliwa mwaka jana wakakosa kupata mazao bora baada ya wengi wao kupata nusu ya gunia ya mbolea waliohitaji.

Menjo alisema kuwa hii itapelekea wakulima wengi wa zao hilo kutelekeza mashamba mengi au hata wagharamike zaidi kutokana na upungufu wa mbolea ya ruzuku kwa kuwa wengi wa wakulima walipanua mashamba yao baada ya bei ya mbolea kurudi chini akitoa wito kwa wizara wa kilimo kuingilia kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *