mwanamme ahukumiwa maisha Jela

Mahakama moja ya Eldoret imemhukumu Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka sabini kifungu cha maisha gerezani kwa kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto msichana mwenye umri wa miaka miwili.

Lukas Umusule anashukiwa kutekeleza kitendo hicho kati ya Mei 21 Mwaka jana na Juni nne  mwaka jana katika mtaa wa Huruma viungani mwa mji wa Eldoret.

Upande wa mashtaka ukiwa na mashahidi wanne akiwemo daktari aliyemfanyia uchunguzi wa matibabu mtoto huyo ulithibitisha kwamba mshukiwa huyo alitekeleza kitendo hicho cha unyama dhidi ya mtoto huyo kwa kumnajisi mara kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa ya mashtaka ya Umma DPP ni kwamba mshukiwa hapo awali alikua amehukumiwa kifungo cha maisha na miaka 40 jela kwa makosa ya unajisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *