Afisa mkuu anayewasimamia maafisa wa jiji maarufu kanjo katika kaunti ya Uasin Gishu Cosmas Kerich amekana madai kwamba maafisa hao wanakwenda kinyume na haki za kibinadamu wakati wanatekeleza jukumu lao.
Akizungumza na wanahabari afisini mwake,afisa huyo amesema kila muda wanapoendelesha opareshini zao wanatekeleza kwa mujibu wa haki na sheria zizazoongoza idara hiyo.
Amesema kwamba maafisa wake wamekuwa wakiendelesha opareshini nyingi za kuleta mpangilio kwenye mji wa Eldoret huku akiongeza kwamba wamefanikiwa kama idara kukabiliana ipasavyo na wafanyibiashara wanaondeleza uuzaji wa dawa za kulevya na hata kuwasaidia vijana wengi kukwepa mitego ya kuwa watumiaji wa madawa hayo.
Kerich ameongeza kwamba wamesaidia mji kuwa na mpangilio kutokana na wafanyibiashara ambao hawa maduka na kurandaranda wakiuza bidhaa zao swala analosema halistahili kwani kila mfanyibiashara anapaswa kuwa na eneo la kuuzia bidhaa zake kwa zoezi hilo kuwa la maendeleo.