Jukumu la wakenya kupata amani nchini ni la serikali na hivyo haja ya serikali kuwahakikishia wenyeji usalama hasa katika maeneo tata yanayoshuhudia utovu wa usalama.
Haya ni kwa mujibu wa Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ambaye amesema kwamba serikali inapaswa kuweka imara hali ya usalama katika ukanda wa kaskazini mwa bonde la ufa ndipo wenyeji maeneo hayo waweze kurejea katika shughuli zao za kawaida.
Askofu Kimengich amesema kwamba inasikitisha kwamba serikali imewatuma maafisa wa usalama katika maeneo yanayoshuhudia utovu wa usalama North Rift ila hali ingali tete swala analosema sharti lishughulikiwe mara moja maana wenyeji wanaumia sana
Aidha,askofu Kimengich amewata wenyeji nao kuwa tayari kukumbatia mwito wa amani akieleza kwamba kunaweza tokea ugumu katika upatikanaji wa amani hiyo iwapo wenyeji hawako tayari kuwatambua wahusika wanaotekeleza uhalifu katika eneo la Kerio Valley.
