Wakulima wanaofuga ng’ombe wa maziwa katika kaunti ya Uasin Gishu wanaitaka sekta ya kilimo kuingilia kati utoaji huduma ya mbegu ya kupatia ng’ombe wa Maziwa kwa kile wanasema huenda ukulima kwa kutumia mbinu ya kupatia Ng’ombe wa kike mbegu maarufu AI.
Wakiongea na wanahabari mjini Eldoret ,wakulima hao walisema wamekuwa wakipata hasara mara si moja kwani huduma hiyo haiku salama kwani ng’ombe hawashiki mimba swala linalowalazimisha kutafuta ndume.
Walisema sharti wizara hiyo itafute mbinu mwafaka wa kuwaokoa wakulima hao la sivyo kilimo kupitia AI haitazaa matunda yoyote.
Wakulima hao hata hivyo walisema kwamba huenda kuna maafisa katika sekta hiyo ambao wanahujumu juhudi za kufanikiwa kwa ukulima kupitia AI wakisema kwamba wanahisi wanapewa mbegu zisizo halali.