Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu imesema imejitolea kuwapa huduma bora wa afya kwa wenyeji huduma ambazo imesema itakua karibu nao.
Kulingana na waziri wa afya katika kaunti ya Uasin Gishu Dkt.Sam Kotut alisema kwamba wizara ya afya imeweka sera na mikakati za kutosha kuhakikisha kila mwananchi anahudumiwa na kupata wahudumu wa kutosha na kando na madawa wanazohitaji.
Aidha,waziri huyo alisema wameshirikiana na washikadau mablimbali hasa wa sekta ya afya kuwafikishia huduma wenyeji karibu na makaazi yao.