Wito umetolewa kwa wazazi kuwa waangalifu na jinsi wanatumia pesa ndipo waweze kuweka akiba ya karo pindi shule zitakapofunguliwa.
Akiongea afisini mwake mjini Eldoret ,pade mkuu wa jimbo katoliki la Eldoret William Kosgei alidokeza kwamba ni jambo la busara wao kutafakari jinsi watakavyo tumia pesa zao wasije wakakwama wakati shule zitakapo funguliwa majuma mawili yajayo.
Vielvile Kosgei alisisitiza haja ya wazazi kuwa makini na kuwakaribia wanao wanapoendelea kufurahia likizo yao ndipo wasijiingize kwenye vikundi vya watoto watundu ambao wanaweza wakawaingiza kwenye utumizi wa mihadarati na maswala mengine yasiyofaa.
Kadhalika,aliwataka watoto nao kuwa wenye heshima kwa wazazi wao na kujitenga na marafiki wasiofaa akiwaeleza kwamba yastahili wafahamu umuhimu wa masomo yao na ndoto wanazotaraji zitatimia kuwa zitatimia iwapo wao wenyewe watajukumika kimaadili.