Papa Francis awataka wanadamu kumtegemea kristu

Baba Francisko amewataka walimwengu kuiga mfano wa mtangulizi wake papa mstaafu Benedict XVI ambaye alikuwa na moyo wa huruma na msamaha.


Akiongea wakati wa ibada ya mazishi ya baba mstaafu Benedict XVI katika uwanja wa mtakatifu Petero mjini Vatican papa Francis amesema kwamba hakuna jambo kizuri kando na mwanadamu kuonyesha huruma kwa wengine kando na kuwaonyesha njia iliyo sawa katika kristu kwa kufuata sheria zake mwokozi na kuwasaidia wengine kuuridhi ufalme wa mbingu.


Papa Francis kadhalika amesifia mtangulizi wake kwa kuwa mwenye kuwa msimamo dhabiti kwa kuwa na moyo wa upendo na msamaha.


Alimiminia sifa marehemu kwa kile alitaja kwamba alionyesha umuhimu wa kuyanyosha mapito kwa kuhubiri neno lake kristu kwa mataifa yote ulimwenguni na kuhakikisha wanadamu wanaunganika kukabiliana na changamoto za maisha kwa kushikana mikono na kuwahimiza wengine kuwa watu wenye uwazi katika maisha.


Misa hiyo ilihudhuriwa na makadinali 120, maaskofu 400 na karibu makasisi 4,000 katika uwanja mkubwa wa Kanisa la Mtakafitu Petro kabla ya mwili wa Benidict wa XVI kuzikwa katika makaburi ya mapapa chini ya kanisa hilo.


Zaidi ya watu 60,000 wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo wajumbe rasmi kutoka Italia na nchini Ujerumani alikozaliwa Benedict, Mfalme na Malkia wa Ubelgiji na wakuu wa nchi au serikali wapatao 13, huku nchi nyengine zikiwakilishwa na mabalozi wao mjini Vatican.


Benedict, ambaye jina la kuzaliwa ni Joseph Ratzinger, alifariki dunia Jumamosi iliyopita akiwa na umri wa miaka 95 ambapo alistaafu kama papa mtakatifu mnamo Aprili mwaka wa 2013 baada ya kuongozaq kanisa katoliki kwa zaidi ya miaka minane na kujiuzulu kwake kulichangiwa na kudoroa kwa hali yake ya afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *