KUPPET YADAI HAKI YA KUPANDISHWA VYEO

Katibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET  tawi la Uasin Gishu  Elijah Maiyo amesikitikia hatua ambayo walimu wanadumu kwa miaka mingi kwenye daraja moja ya ajira swala analosema linachangia walimu wengi kusalia wakiwa walimu wasiokuwa na mishahara za kuridhisha .

Akizungumza mjini Eldoret Maiyo alisema amesikitikia hatua ambayo tume ya kuwaajiri walimu TSC kuwapandisha daraja walimu 31 tu katika kaunti ya Uasin Gishu akieleza wapo walimu wengi ambao wamesalia kwenye daraja moja kwa muda mrefu hata zaidi ya miaka 25 akisema hilo linasikitisha mno.

Wakati huo ,Maiyo akisema utendakazi wa walimu wengi imeathiriwa kwa kukosa matumaini kwa kusalia katika gradi moja miaka nenda miaka rudi na sasa wanatisia kuandamana iwapo haki hizo za kimsingi hazitaangaziwa mara moja.

Alimuomba rais William Ruto kubuni jopo ambalo litashughulikia maslahi ya walimu ndipo maswala ya ukandamizaji ikomeshwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *