KAMISHNA DKT.NYALE:Msihofu lolote usalama u dhabiti

Kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Dkt.Eddyson Nyale amewahakikishia wenyeji usalama wa kutosha msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya.


Akiongea katika kituo cha polisi cha Central Eldoret,Nyale alisema kwamba idara ya usalama iko imara na inaendelea na oparesheni zake za kuhakikisha wenyeji wanaendelea na shughuli zao bila ya hitilafu yoyote.


Nyale aliwatahadharisha wahalifu dhidi ya kujaribu kuharibu usalama kwamba wataadhibiwa vilivyo kwa mujibu wa sheria.


Kadhalika aliwashauri wenyeji kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa zozoze zinazohusiana na watu wanaowashuku kuwa wahalifu kwa hili akisema usalama utaendelea kudumishwa.

Haya yanajiri baada ya maafisa wa polisi kuwakamata washukiwa watatu wa ujambazi wakiwa na bunduki mbili za AK 47 na risasi nne,pamoja na sare bandia za polisi na cheti ghushi cha mamlaka ya uchukuzi wa umma NTSA wanaokisiwa kuwahangaisha wenyeji katika kaunti ya Uasin Gishu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *