NYERI IMEZINDUA MPANGO WA LISHE

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria amezindua mpango wa kuwapa chakula waathiriwa wa baa la njaa katika kaunti saba kwa miezi miwili zijazo.

Mpango huo wenye kauli mbiu hope for you inalenga kuchangisha jumla ya shilingi milioni hamsini kwa lengo la kuwalisha familia zilizoathrika na baa la njaa kwenye kaunti saba, ikiwemo kaunti ya Nyeri, laikipia, Isiolo, marsabit, Kitui, makueni na Samburu,

Askofu mkuu Muheria anasema mpango huo unalenga kuwashirikisha mashirika mbalimbali sisizo za serika,li na zile za serikali kwa miezi miwili zijazo, wakikadiria kwamba wakulimu watakuwa wamevuna mazao yao kwa kipindi hicho.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya baraza la maaskofu nchini KCCB kutoa wito kwa wakenya wenye mapenzi mema pamoja na serikali kujitokeza ili kuwasaidia familia hizo zilizoathirika kote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *