Wito umetolewa kwa wanafunzi kuwa wenye kuaminika katika maisha.
Akiongea wakati wa hafla ya shule za kikatoliki katika shule ya upili ya Bishop Delany Eldoret,askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametaja uaminifu kuwa nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu mwenye hazma na malengo yaliyobora katika maisha.
Vilevile askofu amewakumbusha wanafunzi hao kwamba ni kupitia uaminfu wao wa kweli maisha yao yatakwenda sawasawa katika jamii maana baraka zitawaandama maishani.
Amedokeza kuwa wanafunzi wanapaswa kujikakamua kimasomo ndipo maisha yao ya Usoni isiwe na milima na mabonde kwa hili akitaja kuwa wataafikia malengo yao ya maisha.
