miradi ya maendeleo na wakati

Msemaji wa serikali kanali Cyrus Oguna amewataka wakenya kuwa subra wakati serikali inajizatiti kukamilisha miradi mbalimbali za maendeleo akidokeza kuwa miradi mbalimbali za kiserikali zitakamilika kwa wakati ufaao.

Oguna ametaja kuwepo kwa mikakati kwa kila mradi unaozinduliwa na serikali na akidokeza kuwa miradi hiyo itakamilika kwa muda uloratibiwa.

Akiongea na wanahabari katika kiwanda cha kutengeza nguo cha Rivatex Eldoret amesema kuwa kila jambo lina mpango wake na sharti lifuatiliwa kwa umakini ili uweze kukamilika bila itilafu.

Amewataka wakenya kuwa na imani na viongozi waliowachagua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *